Miaka 10 baadaye, 1928 Jeshi la uingereza lilitoa usamamizi wa mtaa huu kuwa baraza la jiji la Nairobi zama hizo, kauli ambayo ililazimishwa kufutwa kwa nyaraka miliki zote na wakazi wa mtaa huu wakamalizika kutoa stakabadhi za kudhibitisha kwamba wao ni wa asili ya Kinubi. Wanubi hao walitangazwa kuwa maskwota wa serikali ya ukoloni.
Kauli hii ilikuwa na maana kwamba kamishna wa Ardhi alikuwa na uwezo wa kufuta haki ya wa Nubi hao kuwa maswokta katika enelo hilo. Ni kutokana na sababu hii kwamba mijengo yote katika mtaa huu ilikuwa ya muda kwani serikali ilibakia na haki ya kuibomoa wakati wowote na kuitumuia ardhi hiyo kujenga miradi mingine.
Mwaka wa 1948 kulitokea mvuto wa kwanza wa kutaka kuwatimua wakaazi wa mtaa wa Kibera kutokana na msukumo wamatatizo ya kiafya. Licha ya athari za kiafya na ushafuzi wa mazingira, mtaa wa KIbera uliendelea kupanuka na hadi kufikia miaka ya 1970. Idadi ya wakaazi wa mtaa huu ulindelea kuongezeka kwa haraka na mwaka 1980, ulifisika kuwa na idadi kukwa ya watu waliokisiwa kuwa zaidi ya elfu 62,000 kutoka elfu 6,000 tu walikuwepo mwana wa 1965.
Mwaka 1992, mtaa huu ulikuwa naidadi ya watu waliokisiwa kuwa kati ya 248,360 na nusu millioni kufika mwaka 1998. Kulingana na takwimu za hesabu ya watu, mtaa hii ulikuwa unakua kwa asilimia 17 kwa kila mwaka. Suala hili liliekea kuwa kuende mtaa huu ukawa a idadi kati ya watu 700,000 namilioni moja, kukiwa na watu elfu mbili katika kila hekta moja na kati ya watu 3.2 na 4.6 kwa kila chumba kimoja, na hvyo kuufanya mtaa wa Kibera kuwa mkubwa zaidi barani Africa.
Mfumuko wa watu kuhamia mijini wakitokea vijijini umechangia pakubwa kuongezeka kwa idadi ya watu katika mtaa huu. Suala hilo limechangiwa na dhana kwamba jiji la Nairobi likiwa makao makuu ya serikalo, ndipo kuna nafasi nyingi za ajira. Ongeseko la watu katika mtaa wa Kibera, amabako kupangisha chumba ni rahisi kuliko sehemu nyingine yoyote ile jijini, kumechangiwa na kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na ongezeko la idadi ya watu nchini.