Nyumba za mtaa huu ni za matope na ndani yake huwa na vyumba vingi vidogo – vidogo huku zikiezekwa kwa mabati ama debe. Nyumba nyingi za mtaa huu hazina veranda, kuta zake hazipo laini huku barabara zikiwa suala nyeti hususan wakati mtu anapougua kwa haraka. Mianya iliyopo ni vichochoro ambavyo havi pitiki kwa gari. Wakati wa mioto magari hayawezi kufikia sehemu inayoungua. Mifereji michafu iliyo wazi ni jambo la kawaida katika mtaa huu.Tukataka na maji machafu vyote vinatupwa katika mitaro ya mifereji hii. Na wakati takataka hii inapokuwa rundo basi mitaro hiyo huwa imefungwa. Kwa sababu mtaa huu ni sehemu wanakoishi walalao – hio mitaro hii haipo mbali na nyumba nyingi, ndiko mbu wanaosababisha maradhi kibao wanakozaliana.
Licha ya matatizo ya kutokuwa na mitaro ya kuzoa maji taka, wakaati wa Kibera wanakumbana na matatizo mengi likiwepo la uhaba wa safi, elimu, matibabbu na stima. Isitoshe, wakaazi wa mtaa huu wanajikunyata peupe kwa sababu nyumba zao ni za muda tu.
Na mwisho, idadi kubwa ya watu wanao athirikia kutokana na janga la Ukimwi ni tatizo nyeti Takwimu zimebainisha kwamba zaidi ya asilimia 15 ya wakaazi wa mtaa huu wameambukizwa viini vya HIV ama Ukimwi kamili. Idadi hii inaweza kuwa zaidi kwa sabu wengi wao ni watoto wa umri wamiaka mmoja na pengine hawajapima damu. Waathiriwa wengi ni vijana, wazazi na watoto wachanga. Familia nyingi huwa na tatizo kubwa kwa sababu watoto hawa huchangia pakuwabwa kudhoofika kwa afya za wazazi wao huku wao wenyewe wakiiwa hawana usewo wa kujifanya lolote. Wengi wa watoto hawa wameambukizwa viini hivi, lakini sawia na wazazi wao, hawapati huduma zozote na matibabu wala dawa za kukubaliakana na magonjwa nyemelezi na Kurefusha maisha ya waathiriwa.
Ni kutokana na matatizo haya kwamba vijana wa mtaa huu waliungana kubuni SHOFCO kama nguzo imara angalao wakabiliane na baadhi ya matatizo kwa pamoja.